Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwendesha Mashtaka wa Tehran ametangaza kufunguliwa mashtaka dhidi ya idadi ya watu wenye ushawishi wa kisiasa kwa tuhuma za kushirikiana kimtandao na kiuendeshaji na utawala wa Kizayuni pamoja na Marekani. Katika kesi hii, watu 4 wamekamatwa na wengine kadhaa wameitwa kwa mahojiano.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao walihusika wakati wa matukio ya kigaidi ya mwezi Dey, kwa kufanya shughuli zilizopangwa katika mitandao ya kijamii na nyuma ya pazia la kisiasa, kwa lengo la kuhalalisha vitendo vya vurugu, kuchochea misukosuko ya kijamii na kudhoofisha usalama wa ndani wa nchi.
Uchunguzi wa kesi hiyo umewekwa katika ajenda maalumu ya mamlaka ya mahakama.
Your Comment